YALIYO JILI KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI TANGA DHIDI YA YANGA & MGAMBO JKT.
Uwanja wa Mkwakwani Tanga leo palikuwa hapatoshi, Timu ya Yanga walikuwa wakipambana na Mgambo JKT ambao walikutana na timu ya Simba na kuwafunga 2-0, leo ilikuwa zamu ya Yanga na Mgambo.
Dakika 45 za kwanza ziliisha kwa 0-0 lakini waliporudi kumalizia 45 za kipindi cha pili hali ilikuwa tofauti, Yanga waliwazidi nguvu Mgambo na kumaliza dakika 90 za mchezo kwa goli 2-0 ambapo Yanga walitoka kifua mbele kuthibitisha kwamba bado wanahitaji kukaa kwenye kilele cha ligi Kuu Tanzania bara.
No comments:
Post a Comment